Story Book

#MatatuMadness: Ushawahi Skuma Mat Na Umelipia?

By: Kevin Munguti
@KelvinMunguti

Mwalimu kuna siku nilikua na shughuli mingi tu sana baridi ndio hio, mvua kunyesha siku mzima, rasharasha…. jioni ikafika, wakati wakuenda nyumbani, pale stage ya kwetu Embassava sacco ilikua ime-suspendiwa kwa muda kidogo, kunayo hii sacco ingine yajiita Royal swift sacco ndio ilikua ina hudumia wakaazi wote wa Embakasi. Foleni ya kupanda gari ilikua kubwa sana, hapo kwa line niliona wasichana waki rukishwa line bila kupanga na kupewa kiti ya mbele na kutolipa matatu. Mimi naye nimepanga line kwa muda mrefu nika nyeshewa, nikapanda gari kitu 8.30pm ndio tuna toka town, jam ilikua kubwa tuka pita njia ya Eastleigh ya ndani, dereva hakua anajua hio njia ikambidii aongeze sauti ya radio ndio atuchange tusijue tumepotea na hio barabara haitambui.Aliendelea kuguess njia huko tulikuweko, gurudumu ya mbele ya gari ikaingia kwa mtaro. Walijaribu juu chini kututoa hapo lakini wapi, tukaambiwa tukishuka gari ita lighten weight na inaweza toka kwa urahisi, lakini wapi!

Tuko nje ya gari, ni usiku tumechoka, tunanyeshewa na gari iko kwa mtaro. Hizi gari za break down ikapita dereva aka omba kusaidiwa nao walikua wana taka elfu mbili walipwe baada ya kazi…conductor na dereva wakakataa wakisema hio pesa mingi sana kwa hio kazi. Fare ya gari kawaida huwa 70 hio usiku tulilipa 100 na wanakataa kulipa break down watu toke kwa mtaro. Kelele kwa gari “Ooooeeee walipwe pesa yao watutoe kwa mtaro!” Conductor kumbe alishaenda ametuwacha hapo na dereva. Breakdown walitutoa na kulipwa na dereva tuka endelea kwenda nyumbani. Conductor kumbe nikujificha alikua amejificha! Alirudi ndani ya gari na kurushiwa maneno na abiria wengine. Dereva kutu changanya kabisa aka weka wimbo za Kikisii sauti yote kwenye woofer hadi Embakasi. Nilifika nyumbani 12.30am na nilikua nimepanda gari 8.30pm! Umenyeshewa, hakuna magari, umechoka, aaaiiiii!!!

THE END.

Thank you Kevin for contributing your matatu madness story! Totally hilarious! -Mwalimu Rachel.

Leave a Comment